Monday, November 26, 2012

R.I.P SHARO MILIONEA

AFARIKI KATIKA AJARI MBAYA YA GARI, ALIKUA PEKE YAKE KWENYE GARI, AKITOKA DAR KWENDA TANGA.
Marehemu Sharo Milionea

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa mkoa wa Tanga,
Constatine Masawe, Sharo alikuwa peke yake garini wakati ajali hiyo ikitokea na mwili wake uko katika hospitali ya Teule, Muheza. 


Kamanda Masawe alisema Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es Salaam kwenda Muheza alipofika eneo hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake.


Hii ni ajali ya pili kwa Sharo kupata mwaka huu baada ya Januari 5 kunusurika katika ajali ya basi alilokuwa amepanda la Taqwa likitokea Burundi kuelekea Dar es Salaam kupinduka katika eneo Mikese, Morogoro saa mbili na nusu asubuhi.

No comments:

Post a Comment

KUA FAN KUTOKA FACEBOOK, USIPITWE NA HABARI KUHUSU SQUEEZER.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...